1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kuweka mifumo ya ulinzi ya Patriot kwenye ardhi yake

7 Desemba 2022

Poland inajiandaa kuuweka mfumo wa ulinzi wa angani uliotengenezwa Ujerumani unaojulikana kama Patriot kwenye ardhi yake, baada ya Berlin kukataa kuuweka mtambo huo nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Kb1D
Patriot Flugabwehrsystem
Picha: Axel Heimken/dpa/picture alliance

Waziri wa Ulinzi wa Poland Mariusz Blascczak amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuzungumza na Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani.

Amesema kuiweka mifumo hiyo ya Patriot kwenye upande wa magharibi mwa Ukraine kutaimarisha usalama wa Wapoland na Waukraine. Kwa hiyo wameanza mipango ya kuiweka mifumo hiyo ya makombora nchini Poland na kuiunganisha na mifumo ya kamandi ya nchi hiyo.

Ujerumani mwezi uliopita iliipa Poland mfumo wa Patriot ili kuisaidia kuilinda anga yake baada ya kombora kuanguka na kuwauwa watu wawili nchini Poland.

Waziri wa Ulinzi wa Poland baadae akaitaka Ujerumani kupeleka mifumo hiyo nchini Ukraine hatua ambayo Ujerumani iliipinga.