1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PNOM PENH: Wakuu wa Khmer Rouge kushtakiwa Mahakama ya Umoja wa Mataifa

30 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFHz

Serikali ya Cambodia imefurahia tangazo la Umoja wa Mataifa kuwa mahitajio ya kisheria yametekelezwa ili kufungua kesi dhidi ya wakuu wa Khmer Rouge walio hai,takriban miongo mitatu baada ya kuanza mauaji ya halaiki nchini Cambodia.Kuanzia mwaka 1975 hadi 1979,kiasi ya Wacambodia wapato milioni 1.7 ikiwa ni kama theluthi moja ya umma wa nchi hiyo,walipoteza maisha yao kwa sababu ya njaa,kazi ngumu,magonjwa au adhabu ya kifo.