1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiYemen

Pentagon: Boti yenye silaha yakamatwa ikielekea Yemen

2 Februari 2023

Boti iliyokuwa imejaa silaha na vilipuzi zinazodaiwa kupelekwa Yemen kutoka Iran, imekamatwa katika operesheni ya kijeshi ya washirika wa Magharibi iliyoongozwa na Ufaransa

https://p.dw.com/p/4N0QZ
Yemen - al-Hudaida
Picha: picture-alliance/AP Photo/N. El-Mofty

Boti iliyokuwa imejaa silaha na vilipuzi zinazodaiwa kupelekwa Yemen kutoka Iran, imekamatwa katika operesheni ya kijeshi ya washirika wa Magharibi iliyoongozwa na Ufaransa.

Jeshi la Marekani lilisema jana kuwa zaidi ya bunduki 3,000 za kivita, risasi 578,000 na makombora 23 zilikamatwa katika operesheni ya Januari 15 iliyofanika kwenye Ghuba ya Oman.

Kamandi Kuu ya Marekani inayofuatilia shughuli za kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati, imesema operesheni hiyo ilifanyika katika njia ambayo kihistoria inatumika kusafirisha kimagendo silaha kutoka Iran kwenda Yemen.

Januari 6, vikosi vya Marekani viliikamata boti ya uvuvi katika Ghuba ya Oman ambayo ilikuwa imepakia zaidi ya bunduki 2,100 za kivita, zinazoaminika kwamba zilikuwa zikipelekwa Yemen kutoka Iran. Iran imekuwa ikiwaunga mkono waasi wa Kihouthi nchini Yemen.