1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Pengo kati ya mataifa tajiri na maskini latishia umaskini

18 Julai 2023

Mkuu mpya wa Benki ya Dunia Ajay Banga, amesema pengo linalozidi kati ya mataifa tajiri na maskini linatarisha kuongeza umaskini katika ulimwengu wa mataifa yanayoendelea.

https://p.dw.com/p/4U5ql
Mkuu mpya wa Benki ya Dunia Ajay Banga
Mkuu mpya wa Benki ya Dunia Ajay BangaPicha: Punit Paranjpe/AFP/Getty Images

Banga ameyasema hayo katika mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka mataifa ya kundi la G20, unaokamilika hii leo nchini India. Mataifa mengi bado yanaendelea kufufuka kutokana na athari za janga la UVIKO-19 na vita vya Urusi nchini Ukraine, ambavyo vilisababisha kupanda kwa gharama za mafuta na vyakula.

Uamuzi wa Urusi kujiondoa katika mkataba wa nafaka watishia mataifa maskini

Mazungumzo ya G20 yamekuja baada ya Urusi kukataa hapo jana Jumatatu, kurefusha makubaliano yanayoruhusu usafirishaji muhimu wa nafaka kutoka Ukraine kupitia bahari Nyeusi, na kuzusha hasira kutoka Umoja wa Mataifa, ambao umeonya kuwa mamilioni ya watu maskini duniani ndiyo watakaolipa gharama.Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Enoch Gondo-ngwana ameonya kuwa uamuzi huo huenda ukaathiri bei za chakula, ambazo zitayagusa zaidi mataifa maskini.