1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paul Mackenzie kufunguliwa mashtaka ya mauaji na ugaidi

16 Januari 2024

Waendesha mashtaka wa Kenya wanakusudia kumfungulia mashtaka ya mauaji na ugaidi kiongozi wa dhehebu tata la kidini Paul Mackenzie pamoja na washukiwa wengine kutokana na vifo vya wafuasi wake zaidi ya 400.

https://p.dw.com/p/4bKL7
Polizisten eskortieren Ezekiel Ombok Odero im Polizeipräsidium in Mombasa
Picha: Stringer/REUTERS

Hii ni baada ya mahakama wiki iliyopita kutishia kumuachilia huru iwapo upande wa mashtaka utashindwa kumfungulia mashtaka mhubiri huyo.

Mackenzie na washukiwa wenzake sasa watakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo mauaji, mauaji ya bila kukusudia na ugaidi.

Mackenzie kusalia kizuizini miezi sita zaidi

Mhubiri huyo wa kanisa la Good News International anadaiwa kuwarubuni wafuasi wake kujizuia kula au kunywa hadi wafe ili kukutana na Yesu Kristo, katika kisa kilichoushangaza ulimwengu.

Mackenzie alikamatwa mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya miili 429 kugunduliwa katika msitu wa Shakahola, kaskazini mwa pwani ya Kenya. Amekaa rumande kwa zaidi ya siku 117 ili kuruhusu wapelezi kufanya uchunguzi wao.