1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Rais Chiraq atoa mwito Iran isifikishwe nbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa

18 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBD

Rais Jacque Chirac wa Ufaransa amewataka viongozi wa nchi zenye uwezo mkubwa duniani wasi ifikishe Iran mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu mpango wake wa nyuklia na wakati huo huo amesema kuwa vikwazo dhidi ya nchi hiyo havina maana.

Pia rais Chiraq ameitaka Iran kusimamisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.

Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za nishati bwana Mohamed al Baradei amesema kuwa ana matarajio makubwa kwa Iran na nchi za Ulaya kuendeleza mazungumzo yaliyokwama kwa muda mrefu.

Bwana el baradei ameyasema hayo katika mkutano wa shirika hilo la kimataifa mjini Vienna Austria.