1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Rais Chirac awatolea wito wafaransa waikubali katiba mpya ya Umoja wa Ulaya

27 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9m

Rais Jacque Chirac wa Ufaransa amewatolea mwito kwa mara ya mwisho wapiga kura kuikubali katiba mpya ya Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika jumapili.

Akitoa hotuba kwa Wafaransa kupitia televisheni ya taifa bwana Chirac amesema iwapo wapiga kura wa Ufaransa wataipinga kura hiyo itaonekana kana kwamba wameipinga Ulaya na hilo huenda likaidhoofisha nchi hiyo.

Uchunguzi uliotolewa hapo jana unaonyesha kwamba kura ya kuipinga katiba hiyo inaungwa mkono na asilimia 55 ya Wafaransa.

Kura ya Ufaransa ya kuipinga katiba hiyo huenda ikaingamiza katiba hiyo kwani inahitaji kukubaliwa na mataifa yote 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya ili iweze kutumika.