1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Washukiwa ugaidi wakamatwa Ufaransa

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImO

Watu 5 wanaoshukiwa kuhusika na itikadi kali za kiislamu wamekamatwa na polisi katika mji wa mashariki wa Besancon nchini Ufaransa.Washukiwa hao pia wamenyanganywa idadi fulani ya silaha ikiwa ni pamoja na bastola na bunduki aina ya Kalashnikov.

Kwa mujibu wa polisi,washukiwa wote watano ni raia wa Ufaransa wenye asili ya Kibosnia na walikuwa na njama ya kufanya shambulizi la kigaidi.Hapo awali,polisi iliwakamata watu 7 lakini wawili wameachiliwa huru.Wote walitumia msikiti wa mjini Besancon na walikuwa wakichungzwa tangu miaka kadhaa.