1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Wapiga kura wachagua bunge jipya nchini Ufaransa

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBr1

Wapiga kura nchini Ufaransa hii leo wanachagua wabunge wapya katika duru ya pili ya uchaguzi.Hii leo,ni viti 467 vinavyogombewa.Kama ilivyokuwa katika duru ya mwanzo ya uchaguzi juma moja lililopita,chama cha kihafidhina cha UMP cha Rais Nicolas Sarkozy,kinatazamiwa kupata uwingi mkubwa bungeni.Hivyo,Sarkozy aliechaguliwa hivi karibuni ataweza kufanya mageuzi aliyoahidi,ambayo yalimsadia kushinda uchaguzi wa rais,mwezi uliopita.Miongoni mwa mabadiliko aliyoahidi,ni kupunguza kodi katika jitahada ya kupiga jeki ukuaji wa kiuchumi na kuongeza nafasi za ajira. Matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa leo yanatazamiwa kutangazwa,baada ya kufungwa kwa vituo vya mwisho vya kupigia kura katika miji mikubwa,hapo saa mbili za usiku.