1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS-Wafaransa wakikataa katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.

30 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8e

Wapiga kura nchini Ufaransa wameikataa katiba ya Umoja wa Ulaya.Kwa mujibu wa matokeo rasmi ya kura hizo za maoni zilizopigwa jana Jumapili,kiasi cha asilimia 55 wameonesha kukataa kuidhinisha katiba hiyo.Ni aslimia 45 ya wapiga kura ndio wameikubali.

Katiba hiyo mpya iliyoundwa kwa ajili ya kurahisisha upitishwaji wa maamuzi ya Umoja wa Ulaya,hivi sasa ipo mashakani kwa vile haitoweza kutumika hadi mataifa yote 25 wanachama watakaporidhia.

Rais wa Ufaransa,Jacques Chirac amesema baada ya matokeo hayo kutolewa,kuwa kwa Wafaransa kuikataa katiba hiyo,kunahatarisha maslahi ya nchi hiyo na kuna fununu ya kutokea mabadiliko katika baraza la Mawaziri wa nchi hiyo.

Kabla ya kura hiyo kupigwa mataifa tisa ya Umoja wa Ulaya yalikwishaidhinisha katiba hiyo ikiwemo Ujerumani.

Keshokutwa siku ya Jumatano raia wa Uholanzi nao watakuwa katika hekaheka ya kupiga kura ya maoni ya katiba hiyo iwapo wanaiafiki ama la.

Uchunguzi unaonesha mashaka yametapakaa katika kuamua hatma ya katiba hiyo.