1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ufaransa na Comoro kuwa na uhusiano mpya

1 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFdo

Ufaransa na visiwa vya Comoro zimesema hapo jana kwamba zinataraji kuupa uhai mpya uhusiano wao ulioharibika katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kutokuwepo kwa utulivu wa kisiasa katika visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi.

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa na kiongozi wa Comoro Azali Assoumani walikutana mjini Paris katika ziara ya kwanza rasmi nchini Ufaransa kuwahi kufanywa na kiongozi wa Comoro tokea nchi hiyo ijipatie uhuru wake miaka 30 iliopita.

Assoumani kufuatia mkutano wake wa saa moja na Chirac amekaririwa akisema wamezungumzia juu ya uhusiano kati ya Ufaransa na Comoro ambao lazima uamshwe upya na kuimarishwa katika ngazi itakayowafaa.