1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Ufaransa kutohudhuria kikao cha kujadili jeshi la kulinda amani Lebanon.

2 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPV

Ufaransa imesema kuwa haitahudhuria katika mkutano wa kesho katika umoja wa mataifa utakaojadili juu ya jeshi la kimataifa litakalosaidia kuimarisha hali katika eneo la kusini mwa Lebanon.

Waziri wa mambo ya kigeni Philippe Douste-Blazy ameliambia gazeti la Le Monde kuwa Ufaransa haitaki kujadili juu ya jeshi la kimataifa hadi pale makubaliano ya kisiasa ya kumaliza mapigano yatakapokuwepo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ameitisha mkutano huo baada ya kuwa na kikao na mabalozi wa mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, Uinhereza, China , Ufaransa, Urusi na Marekani.