1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ufaransa kukiongoza kikosi cha kimataifa hadi Februari

17 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDKw

Ufaransa imesema iko tayari kukiongoza kikosi cha wanajeshi wa kimataifa watakaolinda amani kusini mwa Lebanon hadi Februari mwaka ujao.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Michele Alliot Marie, amesema kikosi hicho kinatakiwa kiwe na mamlaka iliyo wazi na uwezo wa kutosha kukabiliana na matatizo yatakayotokea.

Kwa mujibu wa ripoti zilitolewa na vyombo vya habari, Italy, Hispania na Finland pia zimekubali kuwatuma wanajeshi wao kwenda Lebanon.

Baadaye leo kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel, anatarajiwa kuwasilisha bungeni mawazo ya serikali yake juu ya kuwahusisha wanajeshi wa Ujerumani katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon.