1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy kuitembelea Libya

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfT

Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, leo anasafiri kwenda Tripoli Libya kufanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Muamar Gaddafi.

Rais Sarkozy alitangaza atafanya ziara yake ya kisiasa nchini Libya baada ya juhudi za Ufaransa kuchangia juhudi za kuachiliwa huru wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa Kipalestina.

Wataalmu hao wa afya wamekuwa wakizuiliwa nchini humo tangu mwaka wa 1999 kwa madai kwamba waliwaambukiza watoto zaidi ya 400 virusi vya ukimwi.

Wachambuzi wanasema Libya yenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi huenda ikawa mshirika muhimu wa kibiashara wa Ufaransa.