1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Rais wa Ufaransa apelekwa hospitali

4 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEec

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 72,amepelekwa hospitali ya kijeshi mjini Paris akiwa na matatizo ya mshipa wa damu na kuathiri uwezo wake wa kuona.Msemaji wa rais Chirac,amesema mikutano yote ya wiki ijayo imefutwa kuambatana na ombi lake.Hakuna cho chote kilichotajwa kuhusu suala la kukabidhi madaraka kwa muda.