1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Raia wa Ufaransa wanapiga kura katika kura ya maoni ya kuidhinisha katiba ya Ulaya leo.

29 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF92

Raia wa Ufaransa wanaoishi nje ya nchi wameanza kupiga kura katika kura ya maoni inayofanyika katika nchi hiyo kuhusu katiba ya umoja wa Ulaya.

Viongozi wa nchi kadha za Ulaya wamejiunga na serikali ya Ufaransa kuwataka wapiga kura wa nchi hiyo kupiga kura ya kuikubali katiba ya umoja wa Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika leo Jumapili, badala ya kutumia kura zao kuipelekea ujumbe wa kuiadhibu serikali yao.

Raia wa Ufaransa wamekuwa zaidi na zaidi na hasira kuhusiana na kiwango kikubwa cha watu wasio na kazi na sera mbaya za soko la kazi.

Katika kura ya maoni , wapiga kura wengi wanasema kuwa wanapanga kuikataa katiba ya umoja wa Ulaya.

Katiba hiyo inahitaji kuidhinishwa na mataifa yote 25 wanachama ili kuweza kupata uwezo wa kufanya kazi.

Siku ya Ijumaa , Ujerumani ilikuwa nchi ya tisa ya umoja wa Ulaya kuidhinisha katiba hiyo baada ya bunge kuu la nchi Bundesrat, kupiga kura ya kuikubali katiba hiyo.