1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS Mwandishi habari wa Ufaransa aliyeachiliwa huru Irak awasili Paris

13 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF49

Mwandishi habari wa kifaransa aliyekuwa akizuiliwa mateka nchini Irak kwa miezi mitano amewasili nchini Ufaransa salama wa salmin. Florence Aubenas aliwasili kwa ndege ya serikali kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi karibu na mji wa Paris.

Mwandishi habari huyo mwenye umri wa miaka 44 anayeripotia gazeti la Liberation alilakiwa na rais wa Ufaransa, Jacques Chirac na jamaa zake.

Aubenas na mkalimani wake muiraki walitekwa nyara baada ya kuondoka hotelini mwao mjini Baghdad mapema mwezi Januari mwaka huu. Wote wawili waliachiliwa huru mnamo Jumamosi iliyopita na mkalimani huyo tayari amejiunga na jamii yake mjini Baghdad.