1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Kufuatia Ujerumani, Ufaransa nayo haitengi tena ...

17 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFiT
uwezekano wa kuisaidia Irak lakini chini ya serikali iliyochaguliwa ya nchi hiyo. Waziri wa kigeni Dominique de Villepin alitamka mjini Paris, serikali yake inachunguza msaada huo uwe katika sekta ya utoaji mafunzo ya askari polisi, baada ya kukabidhiwa madaraka Wairak. Ufaransa , sambamba na Ujerumani na Urussi, iliongoza kundi la nchi zilizopinga vita vya Irak, jambo ambalo lilipekelea kudorora uhusiano na serikali ya Marekani. Kwa mujibu wa gazeti Le Mond, rais Jacque Chirac anazingatia hivi sasa kujiunga na majeshi ya usalama, lakini yaliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa, baada ya kukaliwa Irak. Serikali ya Ujerumani, kama ilivyoarifu, haina nia ya kutuma askari jeshi katika nchi hiyo.