1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Kansela wa Ujerumani na rais wa Ufaransa wakutana mjini Paris.

26 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJ7

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac na kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder wamekuwa na mazungumzo ya kisiasa katika mkutano mjini Paris.

Viongozi hao wawili wanatumia nafasi hiyo , ambayo inaingiliana na maadhimisho ya miaka 50 ya baraza la kibiashara kati ya Ujerumani na Ufaransa, ili kutafuta kuungwa mkono kwa katiba ya jumuiya ya Ulaya.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kulenga katika sera za viwanda kati ya nchi hizo, teknolojia ya habari na usalama , pamoja na kura ya maoni itakayofanyika mwezi ujao kuhusiana na katiba ya jumuiya ya Ulaya.

Kura ya maoni iliyofanyika hivi karibuni inaonesha kuwa wapiga kura wengi wa Ufaransa wanapinga katiba ya umoja wa Ulaya, lakini wanaounga mkono kura hiyo ya hapana wanazidi kupungua. Uchunguzi unaonesha kuwa wapiga kura wa mrengo wa shoto wanapinga katiba hiyo.

Baadaye leo kansela Schroeder atasafiri hadi Poland kwa mazungumzo yasiyo rasmi na serikali ya nchi hiyo.