1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Ghasia zinaendelea nchini Ufaransa.

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKy

Maafisa nchini Ufaransa wanajiweka tayari kwa ajili ya ghasia zinazoweza kuanza tena upya kutokana na ghasia hizo kuendelea nchi nzima katika siku ya 11 mfululizo.

Jioni ya jana Jumapili polisi 10 walijeruhiwa , wawili kati yao vibaya sana , baada ya watu waliokuwa wakifanya ghasia walipowafyatulia risasi.

Siku ya Jumamosi polisi wamewakamata vijana zaidi ya 300 waliokuwa wakifanya uharibifu ambao walichoma moto magari karibu 1,300 na kuharibu majengo kadha.

Ghasia zilisambaa kutoka kitongoji cha mji wa Paris, ambako ndiko zilikoanzia, hadi katikati ya mji huo pamoja na miji mingine kutoka katika pwani ya bahari ya Mediterranean hadi katika mpaka wa Ujerumani, na kumlazimisha rais Jacques Chirac kuitisha kikao cha dharura cha maafisa waandamizi serikalini.

Chirac amesema kurejeshwa haraka kwa utulivu katika jamii ni jambo linalopewa umbele.