1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Ghasia zapungua Ufaransa.

14 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIg

Maafisa nchini Ufaransa wamesema kuwa machafuko ambayo yameendelea nchi nzima kwa zaidi ya wiki mbili yanaonekana kufikia kikomo.

Viongozi wameripoti magari machache yaliyochomwa moto nchi nzima na mji wa Paris umekuwa shwari licha ya tahadhari iliyopelekea kusambazwa kwa polisi kadha wa kuzuwia ghasia katika mitaa ya mji huo.

Ukubwa wa hali hiyo ya ghasia umepungua tangu pale serikali ilipoweka hali ya hatari siku ya Jumatano, na kuwapa madaraka viongozi wa serikali za mitaa kuweka hatua nyingine za kiusalama kama vile kuwapiga marufuku vijana kutoka nje.

Wakati huo huo , rais wa tume ya Ulaya Jose Manuel Barosso amependekeza kuwa umoja wa Ulaya utoe Euro milioni 50 kwa Ufaransa kuweza kusaidia kupeleka nafasi za kazi katika maeneo ya vitongoji vya miji pamoja na kusaidia jamii.