1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Ghasia zaendelea nchini Ufaransa.

13 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIu

Maafisa wa Ufaransa wanasema kuwa magari yamechomwa moto mjini Toulouse na Lyon , katika usiku wa 17 wa machafuko na uharibifu nchini humo.

Hakuna hali ya ghasia iliyoripotiwa katika mji wa Paris, ambako polisi wamesambazwa kwa wingi wakiwa tayari kupambana na uwezekano wa mashambulizi katika maeneo nyeti kama mnara wa Eiffel, ambao ni alama muhimu ya taifa hilo.

Mikusanyiko yote ya hadhara inayoonekana kuwa na uwezekano wa kutokea ghasia imepigwa marufuku hadi Jumapili asubuhi baada ya kutokea miito ya kufanya ghasia , inayoonekana katika mtandao wa internet pamoja na ujumbe katika simu za mkononi.

Maafisa pia wameweka amri ya kutotembea usiku mwishoni mwa juma katika miji kumi ya kusini mashariki ya Ufaransa, wakiwapiga marufuku vijana kutotoka nje bila ya uangalizi wa wazazi wao.