1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Tabia NchiPapua New Guinea

Zaidi ya watu 2,000 wafukiwa na udongo Papua New Guinea

27 Mei 2024

Zaidi ya watu elfu 2 wamefukiwa huko Papua New Guinea kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyokiharibu kijiji kimoja, hatua iliyopelekea serikali kutoa wito wa usaidizi wa kimataifa katika juhudi za uokoaji.

https://p.dw.com/p/4gKC5
Papua-New Guinea | Maporomoko ya ardhi kwenye mkoa wa Enga
Wenyeji wakiwa katika eneo kulikotokea maporomoko ya udongo katika kijiji cha Mulitaka huko Maip Mulitaka, Mkoa wa Enga wa Papua New Guinea Mei 26, 2024.Picha: STR/AFP/Getty Images

Zaidi ya watu elfu 2 wamefukiwa huko Papua New Guinea kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyokiharibu kijiji kimoja, hatua iliyopelekea serikali kutoa wito wa usaidizi wa kimataifa katika juhudi za uokoaji.

Katika barua ya kituo cha kitaifa cha kukabiliana na majanga nchini humo kwa Umoja wa Mataifa, maporomoko hayo yamewafukia watu hao wakiwa hai na kufanya uharibifu mkubwa wa majengo, mashamba na kuuathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo.

Ubalozi wa Ufaransa mjini Port Moresby umesema kwamba Umoja wa Mataifa umeitisha kikao kwa njia ya video hapo kesho kujadili hatua za kuisaidia nchi hiyo.

Wakaazi na vikosi vya uokozi wamekuwa wakitumia machepeo na mbao kuwatafuta waliofukiwa na maporomoko hayo.

Kijiji hicho kilichoko eneo la milimani katika mkoa wa Enga, nusra kisambaratishwe mapema siku ya Ijumaa baada ya sehemu ya Mlima Mungalo kuporomoka na kufunika nyumba na watu kadhaa waliokuwa wamelala.