1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndonesia

Papa, Imamu wa Indonesia waonya dhidi ya uchochezi wa kidini

5 Septemba 2024

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis na Imam Mkuu wa Indonesia Nasaruddin Umar wametia saini tamko la pamoja juu ya kuhimiza utangamano wa dini.

https://p.dw.com/p/4kIiv
Indonesia | Papa Francis mjini Jakarta
Papa Francis na Imamu Mkuu wa Indonesia Nasaruddin Umar wahimiza utangamano wa kidiniPicha: VATICAN MEDIA/Catholic Press Photo/ipa-agency/IMAGO

Papa Francis ametahadharisha dhidi ya kutumia dini kwa lengo la kuchochea migogoro.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki anayemaliza ziara nchini Indonesia alitia saini tamko hilo kwenye msikiti wa Istik-lal mjini Jakarta na pia alikutana na viongozi wa dini sita nchini Indonesia.

Papa Francis amesema kwenye msikiti huo mkubwa kabisa katika eneo la kusini mashariki mwa bara la Asia, watu wote ni ndugu na waumini waliomo njiani kuelekea kwa mwenyezi Mungu.

Amesema binadamu wanakabiliwa na mgogoro mkubwa uliosababishwa na vita na kuharibiwa kwa mazingira.

Papa Francis atamaliza ziara ya nchini Indonesia kwa kuongoza misa, ambapo waumini wapatao 80,000 wanatarajiwa kuhudhuria kwenye uwanja mkuu wa kandanda na kisha ataelekea katika nchi za Papua New Guinea, Timor Mashariki  na Singapore.