Papa Francis awasalimu wakimbizi Vatican
18 Machi 2023Amepongeza matamanio ya wakimbizi hao ya kutaka kuishi mbali na hofu na ukosefu wa usalama.
Papa Francis mwenye miaka 86 amewashukuru pia wote waliowasaidia wakimbizihao katika kuanza maisha mapya akisema kuwakaribisha ni hatua muhimu kuelekea kupata amani. Alitoa salamu kwa takribani watu 6,000 wakiwemo wakimbizi kutoka Syria, Iraq, Afghanistan, Somalia, Sudan Kusini, Libya na Ukraine.
Soma zaidiPapa atoa wito wa kusitishwa kwa safari za vifo
Njia salama za misaada ya kiutu ni mpango ulioanzishwa ili kupata mbadala wa njia ya bahari ambayo tangu mwaka 2014 imesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000. Njia hizo salama ni mpango wa serikali za Ulaya zilizokubaliana kutoa hati za kuingia kwenye mataifa yao na kisha mashirika ya wahisani huzitumia kuwaleta watu walio katika mazingira magumu zaidi wakiwemo watoto na wazee.