1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis atuma ujumbe kwa China akiwa Mongolia

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ametuma ujumbe kwa China na kuwataja raia wa nchi hiyo kuwa watu waungwana huku akiwatolea mwito Wakatoliki wa nchi humo kuwa wakristo na raia wema.

https://p.dw.com/p/4Vtv1
Mongolia | Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis akiendesha ibada MongoliaPicha: Ng Han Guan/AP/picture alliance

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ametuma ujumbe kwa China na kuwataja raia wa nchi hiyo kuwa watu waungwana huku akiwatolea mwito Wakatoliki wa nchi humo kuwa wakristo na raia wema.

Papa Francis ametamka hayo wakati alipokuwa akihitimisha Misa katika mji mkuu wa Mongolia, Ulaanbaatar, anakofanya ziara tangu siku ya Ijumaa. Ujumbe wake kwa China, taifa la kikomunisti unatizamwa kama harakati za kuitaka China kupunguza vikwazo vya kidini.

Katika ziara yake ya Mongolia, ambayo itakamilika kesho Jumatatu, Papa Francis amekutana na jumuiya ya Wakatoliki ambayo idadi yake inafikia waumini takribani 1,450.

Katika matamshi aliyoyatoa jana ambayo yalionekana kuilenga China badala ya Mongolia, Francis alisema serikali hazipaswi kuwa na hofu na Kanisa Katoliki kwa sababu halina ajenda ya siasa.