1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Papa Francis aomboleza kifo cha "raia wasio na ulinzi" Gaza

18 Desemba 2023

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ametumia neno "ugaidi" kuelezea vitendo vya jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4aHHZ
Mji wa Vatican | Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa FrancisPicha: Riccardo De Luca/UPDATE IMAGES PRESS/MAXPPP/dpa/picture alliance

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na mauaji yaliyoripotiwa ya wanawake wawili Wakristo ambao walikuwa wametafuta hifadhi katika majengo ya kanisa kabla ya kuuawa.

Katika hotuba yake ya kila wiki, kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ameeleza kuwa "raia wasio na ulinzi" wanalengwa kwa kupigwa risasi na kushambuliwa kwa mabomu.

Ameendelea kueleza kuwa, wanawake hao waliuawa na "wadunguaji" na kwamba nyumba ya watawa iliyoanzishwa na Mama Teresa pia iliharibiwa na makombora ya Israel.

Papa Francis pia ametoa wito wa kusitisha mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas uliozuka tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kufanya shambulio ndani ya ardhi ya Israel.