1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa Francis alazwa hospitali ili kufanyiwa upasuaji

7 Juni 2023

Kiongozi wa Kanisa Katolika duniani Papa Francis amelazwa hosptiali ili kufanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili tangu alipopata maradhi yaliyolazimisha madaktari kuondoa sehemu ya utumbo wake mkubwa.

https://p.dw.com/p/4SJQG
Papst Franziskus
Picha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Taarifa kutoka makao makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican, imesema Baba Mtakatifu amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya tumbo kwenye kovu la upasuaji wa mwaka 2021.

Hii leo Papa Francis alifikishwa kwenye hospitali ya Gemelli mjini Roma anakotarajiwa kufanyiwa upasuaji huo wa tumbo na atabakia hospitali kwa siku kadhaa zinazokuja.

Katika miezi ya karibuni, hali ya afya ya kiongozi huyo wa kidini limekuwa suala la mjadala hususani juu ya uwezo wake wa kimwili wa kuendelea kuwa mkuu wa Kanisa Katoliki lenye zaidi ya waumini bilioni 1.2 duniani.