1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis aiomba Urusi irudi kwenye makubaliano ya nafaka

30 Julai 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameitolea wito Urusi kurejea kwenye makubaliano ya nafaka kupitia Bahari Nyeusi na kuzisambaza kote ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4UYvB
Vatikanstadt | Forderung vom Papst | Wiederaufnahme von Getreide-Abkommen
Papa Francis Picha: Imago Images

Karibu tani milioni 33 za nafaka zilisafirishwa kutoka katika bandari za Ukraine chini ya makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka uliopita, na kupunguza gharama na kitisho cha upungufu wa chakula duniani.

Papa Francis ametoa wito huo katika sala ya Jumapili, akiiomba Urusi kurudi kwenye makubaliano.

Soma zaidi: Papa arejea wito wa kustishwa mapigano Ukraine

Amesema wakati wote wamekuwa wakiwaombea mashahidi wa Ukraine, ambako vita vinaharibu kila kitu, ikiwa ni pamoja na nafaka, akisema ni kosa kubwa mbele za Mungu kwa kuwa nafaka ni zawadi kutoka kwake kwa ajili ya kuwalisha wanadamu.

Urusi imejiondoa kwenye makubaliano hayo wiki mbili zilizopita na imekataa kuongeza muda wake.