1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Papa arejea wito wa kustishwa mapigano Ukraine

22 Februari 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amerejea wito wake wa kutaka kusitishwa kile alichokiita vita vya "kipuuzi na kikatili" nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4NqNE
Vatikan Christmette Papst Franziskus
Picha: Andreas Solaro/AFP/Getty Images

Wito huo ameutoa Jumatano mjini Vatican, katika hadhara yake ya kila juma, ikiwa ni kipindi kifupi kabla ya kutimia mwaka mmoja tangu uvamizi wa Urusi.

Papa mwenye umri wa miaka 86 amesema idadi ya vifo, wanaojeruhiwa, wakimbizi, waliotengwa, uharibifu wa uchumi na kijamii vinajieleza vyenyewe.

Papa amerudia kutoa wito wa kukomesha mzozo huo tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 24, 2022, hata kufikia hatua ya kuonesha nia ya kufanya safari za kwenda Kiev na Moscow, safari ambazo hadi sasa bado hazijafanyika.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amewatolea wito viongozi wote wa mataifa yenye nguvu duniani kufanya juhudi madhubuti kuhakikisha kwamba mzozo huo unamalizika na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanza kwa mazungumzo ya amani.