1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Papa Francis afadhaishwa na kurejea kwa mapigano Gaza

3 Desemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa amefadhaishwa na kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha vita kwenye Ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4Zj6g
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani - Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani - Papa FrancisPicha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Katika ujumbe uliosomwa na msaidizi wake kwenye kanisa kuu la mtakafitu Petro mjini Vatican, Papa Francis amesema "Gaza inapitia masaibu ya kutisha"

Amesema usitishaji mapigano utamaanisha kuwanusuru watu na "vifo, uharibifu na madhila" na kukumbusha kuwa Ukanda wa Gaza unashuhudia upungufu mkubwa wa mahitaji muhimu.

Soma pia: Papa Francis akutana na jamaa za waliotekwa na Hamas na wafungwa wa Palestina

Matamshi  hayo yanafuatia kuanza tena kwa hujuma za Israel kwenye Ukanda wa Gaza baada ya pande mbili, Israel na Hamas kutuhumiana kukiuka masharti ya mkataba wa kusitisha mapigano.

Israel inasema inalenga kulitokomeza kundi la Hamas inalolizingatia kuwa la kigaidi, na ambalo lilifanya shambulizi kubwa mnamo Oktoba 7 na kuwauwa watu 1,200 ndani ya ardhi ya Israel.