1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa asema hali ya demokrasia imedhoofika duniani

7 Julai 2024

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema hali ya demokrasia duniani imedhoofika na kuonya dhidi ya siasa za hamasa na wale wanaopendelea siasa za itikadi kali.

https://p.dw.com/p/4hz9n
Papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis Picha: Alessandra Tarantino/AP Photo/picture alliance

Papa Francis ameyasema hayo kupitia hotuba yake aliyoitoa kwenye mji wa Trieste, kaskazini mashariki mwa Italia wakati akifunga kongamano moja la kikatoliki.

Hotuba ya Papa ameitoa katika wakati Ufaransa inafanya uchaguzi ambao unaweza kukipa wingi mkubwa wa viti bungeni chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally.

Papa Francis akamilisha ziara yake nchini Sudan Kusini na amehimiza juu ya kukomeshwa chuki na ghasia.

Vyama vya siasa za aina hiyo vipo pia madarakani nchini Italia, Hungary na Uholanzi.

Kupata nguvu kwa vuguvugu la vyama hivyo kunaleta hali ya wasiwasi barani Ulaya kutokana na misimamo yao kiitikadi ikiwa ni pamoja na kupinga wahamiaji na kutopendelea mahusiano ya karibu miongoni mwa mataifa.