1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Pande zinazohasimiana Yemen kubadilishana wafungwa

20 Machi 2023

Waasi wa Kihouthi na serikali inayotambuliwa kimataifa wamefikia makubaliano ya kubadilishana wafungwa.

https://p.dw.com/p/4OwZi
Jemen Sanaa | Saudi-geführte Luftangriffe auf Häuser
Picha: Hani Mohammed/AP Photo/picture alliance

Waasi hao wamesena makubaliano yamefikiwa leo wakati wa mazungumzo yaliyofanyika nchini Uswisi. Kiongozi wa Kihouthi aliyeongoza ujumbe wa waasi hao, Abdul Qader al-Murtada amesema zaidi ya watu 880 wataachiwa huru.

Al-Murtada ambaye pia anaongoza Kamati ya Kitaifa ya Masuala ya Wafungwa, amesema kulingana na makubaliano hayo, waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, watawaachia huru wafungwa 181, wakiwemo raia wa Saudi Arabia na Sudan, katika kubadilishana wafungwa 706.

Soma pia: Pande mbili zinazozozana Yemen zaanza mazungumzo

Makubaliano hayo yatatekelezwa baada ya wiki tatu. Mazungumzo hayo yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, ICRC yalianza mwezi huu.