1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaPakistan

Pakistan yagundua aina ndogo ya kirusi cha Omicron

3 Januari 2023

Taasisi ya taifa ya afya nchini Pakistan imethibitisha kugundulika kwa aina nyingine ndogo ya kirusi cha Omicron XBB.

https://p.dw.com/p/4Lh4P
German Africa Prize in 2022 Covid-19 Omicron Variante
Picha: DW

Waziri mkuu Shehbaz Sharif amekagua utayari wa mamlaka katika kukabiliana na uwezekano wa kusambaa kwa maambukizi mapya ya kirusi hicho.

Waziri huyo amezitaka mamlaka kuimarisha ukaguzi wa wasafiri katika viwanja vya ndege, mipakani pamoja na kuwachanja watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 12 katika hali ya dharura.

Mataifa yaliyoweka masharti ya kuwapima wasafiri kutoka nchini China ambayo inakabiliana na Covid kwa sasa, yametaja ukosefu wa uwazi wa China kuhusu taarifa za ugonjwa huo na hatari ya kuibuka kwa aina mpya ya virusi kama sababu za kuweka masharti hayo.

Pakistan imerekodi zaidi ya visa milioni 1.5 na vifo 30,000 vinavyohusiana na janga la Covid-19 tangu kuzuka kwake.