1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan yafunga kivuko cha mpakani na Afghanistan

7 Septemba 2023

Pakistan imekifunga kivuko muhimu cha mpakani na Afghnistan kufuatia machafuko.

https://p.dw.com/p/4W2Rk
Afghanistan | Taliban feiern zwei Jahre seit ihrer Rückkehr an die Macht
Picha: Zerah Oriane/Abaca/picture alliance

Pakistan imekifunga kivuko muhimu katika mpaka wa kaskazini magharibi na Afghanistanbaada ya walinzi wa mpakani wa nchi hizo mbili kufyetuliana risasi jana Jumatano. Taarifa ya jeshi la Pakistan imesema makabiliano hayo yalitokea wakati kundi kubwa la magaidi waliojihami na silaha za kisasa katika wilaya ya kaskazini ya Chitral inayopakana na Afghanistan walipovishambulia vituo viwili vya jeshi la Pakistan.

Taarifa hiyo pia imesema wanajeshi wanne wa Pakistan na wanamgambo 12 waliuwawa katika machafuko hayo. Maafisa hawakutoa maelezo kuhusu wanamambo hao lakini wamependekeza huenda wana mafungamano na nchi jirani ya Afghanistan.

Taarifa ya jeshi imesema Pakistan inatarajia serikali ya Taliban nchini Afghanistan itimize majukumu yake na iwazuie magaidi kuitumia adhi ya Afghanistan kupanga vitendo vya kigaidi dhidi ya Pakistan.