1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Pakistan wapiga kura kuchaguwa wabunge

8 Februari 2024

Raia milioni 127 wa Pakistan hii leo wanapiga kura kuwachagua wabunge, huu ukiwa ni uchaguzi wa 12 katika historia ya taifa hilo ya miaka 76 iliyogubikwa na mizozo ya kiuchumi, kijeshi, na kisiasa na vita na India.

https://p.dw.com/p/4c9vQ
Uchaguzi wa Pakistan
Maafisa wa uchaguzi wakisambaza vifaa vya uchaguzi nchini Pakistan.Picha: BANARAS KHAN/AFP

Vyama vya kisiasa 44 vinawakilishwa na wagombea wao katika vuta nikuvute ya kuwania viti 266 vya Bunge la Kitaifa ama baraza la wawakilishi lenye vita vya ziada 70 vilivyotengwa kwa ajili ya wanawake na jamii za walio wachache.

Baada ya uchaguzi, bunge jipya litamchagua waziri mkuu. Na kama hakutakuwa na mshindi aliyepata wingi wa kutosha wa kura, mgombea mwenye kura nyingi anaweza kuunda serikali kwa ushirikiano na vyama vyengine.

Jana Jumatano, ofisi mbili za wanasiasa zilishambuliwa kwa mabomu kusinimagharibi mwa Pakistan na kuwaua watu 30.