1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Pakistan: Imran Khan afunguliwa mashtaka ya ugaidi.

19 Machi 2023

Polisi katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad wamefungua mashtaka ya ugaidi na makosa mengine dhidi ya Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Imran Khan.

https://p.dw.com/p/4OuH4
Pakistan | Imran Khan | ehemaliger Premierminister
Picha: Akhtar Soomro/REUTERS

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Pakistan, Imran Khan aliyeondolewa madarakani mwezi Aprili mwaka jana baada ya Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Mashtaka hayo ya ugaidi na mengineyo yanawakabili pia wasaidizi wake 17 pamoja na wafuasi wake ambao siku ya Jumamosi walikabiliana na polisi mjini Islamabad, nje ya Mahakama ambako Khan alitakiwa kusikiliza kesi ya ufisadi dhidi yake.

Zaidi ya maafisa 50 walijeruhiwa huku kituo cha polisi, magari na pikipiki kadhaa zikichomwa moto. Polisi wamesema wafuasi wapatao 59 wa Khan walikamatwa wakati wa vurugu hizo.

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan amekuwa akipinga hatua ya kung'olewa kwake madarakani akisema ilikuwa njama ya mrithi wake Shahbaz Sharif akisaidiwa na Marekani.