1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Ousmane Sonko, awasilisha ombi la kuwania Urais Senegal

26 Desemba 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal aliyefungwa jela Ousmane Sonko, amewasilisha kwa baraza la katiba azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa Februari licha ya serikali kukataa kumpa nyaraka zinazohitajika.

https://p.dw.com/p/4aamk
Senegal Dakar
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, wakiwa wamebeba bendera na picha ya Sonko mjini Dakar.Picha: JOHN WESSELS/AFP/ Getty Images

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal aliyefungwa jela Ousmane Sonko, amewasilisha kwa baraza la katiba azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa Februari licha ya serikali kukataa kumpa nyaraka zinazohitajika.

Chama cha upinzani kilichofutwa, kimesema mgombea anayeshirikiana na Sonko, Bassirou Diomaye Faye ambaye pia yuko gerezani amewasilisha ombi la kugombea. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni leo tarehe 26 Desemba.

Soma pia: Senegal: Mahakama yaamuru jina la kiongozi wa upinzani kurejeshwa kwenye daftari la uchaguzi

Sonko anakabiliwa na msururu wa kesi mahakamani katika muda wa miaka miwili iliyopita kwa mashtaka ya kuchochea uasi, kula njama na makundi ya kigaidi, na kuhatarisha usalama wa nchi miongoni mwa mengine.

Sonko mwenye umri wa miaka 49 amekanusha tuhuma hizo akisema ni njama ya kumzuia kumpinga RaisMacky Sall katika uchaguzi wa Februari 25.