1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OUJDA : Wahamiaji wa Kiafrika waanza kurudishwa makwao

10 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CET9

Morroco ikiwa kwenye kitovu cha mgogoro wa wahamiaji wa Kiafrika wanaotaka kukimbilia Ulaya imeanza kuwarudisha makwao wahamiaji hao leo hii kwa kuanza kuwasafirisha kwa ndege Wasenegali 140.

Ndege ya Morocco ya Royal Air Maroc iliondoka Oujda kaskazini mashariki ya Morocco na kuelekea Dakar ikiwa na polisi ndani ya ndege hiyo.Hata hivyo Wasenegali hao walikuwa hawakutiwa pingu.

Mamia ya wahamiaji walikamatwa na polisi ya Morroco na kupelekwa kwenye eneo la jangwani karibu na mpaka wa Algeria baada ya wimbi la wahamiaji kujaribu kuvuka mipaka ya uzio wa sen’gen’ge kutoka Morocco na kuingia kwenye maeneo ya Uhispania ya Melilla na Ceuta yalioko ndani ya mwambao wa kaskazini wa Morocco.

Wahamiaji hao wanasema walikuwa wamekwama katika eneo hilo la jangwani bila ya kupatiwa maji na chakula kwa siku kadhaa hadi pale serikali ya Morocco ilipolazimika kuchukuwa hatua chini ya shutuma nzito za kimataifa kwa kuwachukuwa na kuanza taratibu za kuwarudisha makwao.

Maelfu ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika Magharibi ya Senegal na Mali wamekuwa wakijaribu kukimbilia Ulaya kwa kupitia taifa hilo la Afrika kaskazini.