Makala ya Mwangaza wa Ulaya inaangazia baa la kuongezeka kwa idadi ya watu wasiokuwa na makaazi katika nchi za Ulaya. Jee nini maana ya mtu asiekuwa na makaazi? Jiunge na mtayarishaji Zainab Aziz, atakayekufahamisha kwamba ukweli si watu wote wasiokuwa na maakazi wanalala nje.