1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ongezeko la joto duniani lilipindukia muongo uliopita.

Daniel Gakuba
8 Juni 2023

Ongezeko la joto duniani lilifikia nyuzi 1.14 za Celsius katika kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2022, hayo yakiwa ni kwa mujibu wa utafiti.

https://p.dw.com/p/4SLY2
Moshi mkubwa ukifuka katika msitu ulioko kusinimashariki mwa Canada, karibu na ziwa Alberta.
Shughuli za binadamu zinatajwa kuchangia pakubwa katika ongezeko la joto duniani.Picha: Alberta Wildfire via REUTERS

Ripoti hiyo imetolewa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira unaoendelea mjini Bonn. Ripoti hiyo iliyochapishwa leo katika jarida la data za mfumo wa sayansi ya dunia, inaonesha kuwa shughuli za binadamu zinasababisha joto kupanda kwa nyuzi 0.2 za Celsius kila baada ya muongo mmoja.

Soma Zaidi: Kiwango cha joto duniani kuongezeka kwa nyuzi 1.5 katika miaka 5 ijayo

Katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi, COP28 utakaofanyika kati ya Novemba 30 na Desemba 12 mwaka huu, ulimwengu utatathmini hatua inazozichukua, na kuzilinganisha na malengo iliyojiwekea mjini Paris mwaka 2015. Malengo hayo ni kubakisha ongezeko la joto katika kiwango cha asilimia 1.5 juu ya hali ya kabla ya mapinduzi ya viwanda, la sivyo dunia itakumbwa na majanga.