1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Ofisi ya haki za binaadamu kufungwa Uganda

4 Agosti 2023

Umoja wa Mataifa umefahamisha hii leo kuwa ofisi yake ya haki za binaadamu mjini Kampala nchini Uganda.

https://p.dw.com/p/4UnBe
Uganda Anti LGBTQ Bill
Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Hii ni baada ya serikali kukataa kuurefusha mkataba ambao umekuwa ukiiruhusu taasisi hiyo kufanya kazi nchini humo kwa takriban miongo miwili.

Taaarifa ya Umoja huo imebaini kuwa Ofisi ndogo za Gulu na Moroto tayari zilifungwa katika wiki za hivi karibuni.

soma pia: Umoja wa Mataifa wahofia uvunjwaji haki za binaadamu Uganda

Mkuu wa kitengo cha haki za binaadamu katika Umoja wa Mataifa Volker Turk ametaja kusikitishwa na hatua hiyo akisema kwa miaka 18 wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu na asasi za kiraia, watu wa tabaka mbalimbali pamoja na kushirikiana na taasisi za serikali kwa ajili ya kukuza na kulinda haki za binadamu za raia wote waUganda.

Turk amekosoa pia kuporomoka kwa uhuru wa kujieleza, pamoja na sheria ya ubaguzi iliyoidhinishwa hivi karibuni dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja akisema ina athari mbaya kwa Waganda.