1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Odinga aidhinishwa rasmi na Azimio la Umoja kugombea urais

12 Machi 2022

Rais Kenyatta amemuunga mkono Raila ambaye aliwahi kuwa mpinzani wake ikiwa ni wiki chache baada ya vyama vyao kuunganisha nguvu pamoja kuelekea uchaguzi mkuu wa rais na bunge utakaofanyika Agosti 9

https://p.dw.com/p/48Odp
Kenia Nairobi | Gideon Moi  und weitere
Picha: Shisia Wasilwa/DW

Rais Kenyatta amemuunga mkono Raila ambaye aliwahi kuwa mpinzani wake ikiwa ni wiki chache baada ya vyama vyao kuunganisha nguvu pamoja kuelekea uchaguzi mkuu wa rais na bunge utakaofanyika mwezo Agosti mwaka huu.

Rais Kenyatta amesema wamemchagua Raila Odinga bila ya kupingwa kuwa rais wa tano wa Kenya.

Ni Tamko la Kenyatta alilolitowa Jumamosi hii akishangiliwa na umma wa maelfu ya Wakenya jijini Nairobi. Tangazo hilo linawaleta pamoja vigogo wawili kutoka familia zenye nguvu kisiasa katika nchi hiyo ambao wanahistoria ndefu ya kupingana kwenye sanduku la kura.

Uhuru Kenyatta Präsident Kenia Rede Parlament Nairobi
Rais Uhuru Kenyatta wa KenyaPicha: Simon Maina/AFP via Getty Images

Ingawa mnamo mwaka 2018 Kenyatta na Odinga waliishanga nchi hiyo ya Afrika Mashariki baada ya kunyooshena mikono ya kuonesha kuridhiana na kutangaza kufikia mwafaka wa kusitisha uhasama  baada ya ghasia zilizotokea mara baada ya uchaguzi mnamo mwaka 2017 na watu chungunzima waliuwawa.

Mwanzo wa ishara ya taswira mpya ya siasa za miungano ya Kenya.

Mwezi Uliopita chama cha rais Kenyatta Jubilee kilitangaza rasmi kwamba kitaungana na muungano wa Azimio la Umoja unaoongozwa na Raila Odinga. Na leo Muungano huo umemtangaza rasmi Odinga kuwa mshika bendera wake wa kinya'ng'anyiro cha urais. Rais Kenyatta ameweka wazi leo Jumamosi 12.03.2022 kwamba anamuunga mkono kipngozi huyo mkongwe wa upinzani akisema na hapa namnukuu maneno yake:

''Hatuna shaka ya aina yoyote kwamba kwa Raila Odinga tuna nahodha wa timu''

Odinga mwenye umri wa miaka 77 amekubali uteuzi huo kwa heshima kubwa na kwa kujitolewa kwa dhati kwa wananchi wa Kenya. Na tangazo hili la kuteuliwa Odinga limekuja baada ya William Ruto ambaye ni makamu wa rais na mtu aliyetegemewa kurithi kiti cha urais baada ya Kenyatta kutimuliwa kwenye chama cha Jubilee.