1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Salah kuzikosa mechi mbili za AFCON kutokana na jeraha

20 Januari 2024

Nyota wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah atazikosa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutokana na jeraha la msuli wa nyuma ya paja.

https://p.dw.com/p/4bUbv
AFCON | Misri vs Msumbiji | Mo Salah
Nyota wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah Picha: Kim Price/CSM via ZUMA Press Wire/picture alliance

Shirikisho la soka la Misri limesema katika taarifa kuwa, Salah anayechezea pia klabu ya Liverpool nchini Uingereza, hatopatikana katika michezo miwili ijayo hadi angalau hatua ya robo fainali.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alitoka uwanjani mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika mechi dhidi ya Ghana siku ya Alhamisi iliyokamilika kwa sare ya 2-2.

Hii ina maana kuwa, nyota huyo ataikosa mechi dhidi ya Cape Verde na hatua ya mtoano iwapo Misri itafanikiwa kufuzu robo fainali.

Baada ya kutoka sare katika michezo yao miwili, Misri inahitaji kuifunga Cape Verde ili kuwa na uhakika wa kufuzu katika hatua ya mtoano.