1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUACKCHOTT: Wakimbizi wamenasa jangwani

2 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDG4

Mauritania imekubali kuwaruhusu zaidi ya wahamiaji 50 kutoka nchi za Afrika ya Magharibi kuingia nchini.Watu hao wamenasa jangwani katika eneo la mpakani,tangu kufukuzwa na Morocco juma moja lililopita.Kundi hilo ni sehemu ya Waafrika wanaojaribu kuhamia Ulaya katika boti kwa njia zisizo halali na walinasa kati ya Mauritania na eneo la Sahara ya Magharibi,linalodhibitiwa na Morocco,baada ya kuzuiliwa na nchi zote mbili. Kwa mujibu wa wafanya kazi wa mashirika ya misaada katika eneo hilo la mpakani,M-Mali mmoja amefariki.