1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nikki Haley ang'ang'ania kuwania urais licha kushindwa tena

8 Februari 2024

Mgombea wa urais nchini Marekani Nikki Haley amesema hatajitoa kwenye kinyang'anyiro hicho dhidi ya mpinzani wake Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4c9ue
Marekani | Nikki Haley, Conway
Nikki Haley amesema ataendelea kupigania kuchaguliwa kuwania urais kupitia Republican.Picha: Sean Rayford/SOPA Images/Sipa USA/picture alliance

Kwa mara nyengine, Haley ameshindwa vibaya kwenye kura za mchujo za majimbo, mara hii katika jimbo la Nevada.

Balozi huyo wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa alishindwa katika kura hizo za mchujo kupitia chama cha Republican siku ya Jumanne, ingawa alikuwa mgombea pekee aliyeorodhoshwa.

Msemaji wa Haley, Olivia Perez-Cubas, amepuuza hatua hiyo na kudai zoezi zima lilimpendelea Turmp.

Haley, alipata asilimia 31 tu dhidi ya 63 ya kura ambazo hazikumchagua mgombea yoyote, hii ikiwa ni kulingana na maafisa waliosimamia zoezi hilo huko Nevada.