1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yawaonya raia wake dhidi ya kusafiri kuelekea China

30 Januari 2020

Nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, Nigeria, imewaambia raia wake waepuke kusafiri China kwa karibu wiki mbili hivi kwasababu ya mripuko wa virusi vya Corona.

https://p.dw.com/p/3X3fX
Indonesien Coronavirus
Picha: picture-alliance/Zumapress/A. I. Damnik

Kulingana na waziri wa afya wa nchi hiyo Osagie Ehanire wale wanaorudi Nigeria kutoka China pia wanastahili kujiweka karantini wenyewe kwa kipindi hicho hicho cha wiki mbili.

Ehanire amedai wanaoonyesha dalili za virusi hivyo ndio watakaowekwa katika karantini ya lazima hospitali.

Virusi hivyo ambavyo kitovu chake ni mji wa Wuhan huko China kimesababisha vifo vya watu 170 na visa vya virusi hivyo vikiripotiwa katika nchi nyengine duniani pia.

Hakujathibitishwa kisa chochote cha virusi hivyo barani Afrika ingawa maafisa wa Sudan wameripoti kuwa wameripoti kuhusu watu wawili wanaoshukiwa kuambukizwa.