Nigeria yasema uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa
18 Januari 2023Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria amesema nchi hiyo haitaahirisha uchaguzi mkuu wa mwezi ujao, licha ya wasiwasi juu ya kuzorota kwa usalama na mashambulizi dhidi ya maafisa wa uchaguzi.
Akizungumza mjini London, afisa huyo, Mahmood Yakubu amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imejiandaa vyema kuendesha uchaguzi katika taifa hilo lenye wakaazi wengi zaidi barani Afrika pamoja na changamoto zilizopo.
Raia wa Nigeria watamchagua rais mpya tarehe 25 Februari, atakayechukua nafasi ya rais wa sasa Muhammadu Buhari ambaye muhula wake wa pili na wa mwisho umemalizika. Seneti Nigeria yabadili sheria ya matokeo ya uchaguzi
Nchi hiyo inao wakaazi wapatao milioni 200 na uchumi imara zaidi barani Afrika, na mapambano yake dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali za kiislamu yanatazamwa na wengi kama kigezo muhimu kwa utangamano wa kikanda.