1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Nigeria yajiandaa kwa maandamano kupinga gharama ya maisha

1 Agosti 2024

Nigeria inajiandaa kwa maandamano ya nchi nzima ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha, wakati mamlaka zikionya juu ya jaribio lolote la kuiga maandamano ya vijana wa nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/4izqy
Maandamano ya Nigeria
Wanigeria wanaandamana kulalamikia kuongezeka kwa gharama ya maisha Picha: Adekunle Ajayi/NurPhoto/picture alliance

Nigeria inajiandaa kwa maandamano ya nchi nzima ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha, wakati mamlaka zikionya juu ya jaribio lolote la kuiga maandamano ya vijana wa nchini Kenya, yaliyoilazimisha serikali kuachana na muswada wa fedha, ulioazimia kupandisha kodi.

Soma pia: Jeshi la Nigeria laonya dhidi ya ghasia za mtindo wa Kenya

Maandamano hayo yenye hashtag #EndbadGovernanceinNigeria yamepata uungwaji mkono mkubwa kupitia kampeni ya mitandaoni miongoni mwa raia walioelemewa na gharama za chakula zilizoongezeka kwa asilimia 40 pamoja na bei ya mafuta.

Taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika linakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa sarafu yake ya Naira baada ya Rais Bola Tinubu kuanzisha mageuzi mwaka uliopita yaliyolenga kufufua uchumi uliozorota.