1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaifanyia mageuzi mikataba ya mafuta

5 Novemba 2019

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hapo Jumatatu alisaini hatua za kufanyika mageuzi katika mikataba iliyofikiwa na makampuni ya mafuta kwa lengo la kuongeza kwa kiwango kikubwa kiasi cha mapato kinachochukuliwa na taifa.

https://p.dw.com/p/3SUCH
UN-Generalversammlung in New York | Muhammadu Buhari, Präsident Nigeria
Picha: Reuters/C. Allegri

Rais huyo amesema sasa Nigeria itapokea kiwango inachostahili cha mapato kinachotokana na rasilimali yake ya nishati kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003. Hata hivyo haijakuwa wazi ikiwa hatua hiyo itaanza kutekelezwa mara moja au itafungua mijadala na makampuni ya mafuta kuhusu kupitiwa upya mikataba yao na ofisi ya rais Buhari imekadiria kwamba mageuzi hayo yatatowa fursa ya kupatikana alau dola bilioni 1.5 katika ongezeko la mapato kila mwaka kufikia mwaka 2021.